Unterschiedliche Begriffe von Armut - im Kisuaheli

Mkuu wa mkoa Frank Baranowski na wageni kutoka Morogoro Tanzania wajadiliana juu ya umaskini

Kutoka kushoto: Mchg. Reginald Makule, Frank Baranowski na Ask. Jacob Mameo wakijadiliana kwa pamoja mambo mbalimbali.

Kutoka kushoto: Mchg. Reginald Makule, Frank Baranowski na Ask. Jacob Mameo wakijadiliana kwa pamoja mambo mbalimbali.

Kitabu kinachosainiwa na wageni Schloss Horst.

Kitabu kinachosainiwa na wageni Schloss Horst.

Chumba maalum alichofanyia mazungumzo mkuu wa Mkoa Frank Baranowski na wageni kutoka Morogoro.  Mpiga picha: CORNELIA FISCHER

Tarehe 10. Juni, 2013 wageni 6 toka Morogoro Tanzania walimtembelea mkuu wa mkoa wa Gelsenkirchen ndugu Frank Baranowski ofisini kwake. Aliwapokea kwa furaha na kusema „Ni mara chache walibahatika kutembelewa na wageni toka mbali sana.“  Wakiongozwa na Askofu Jakob Mameo,  walisaini katika kitabu cha wageni cha Schloss Horst makao makuu ya ofisi hiyo ya mkoa.

Mwenyekiti wa Uhusiano wa jimbo la Gelsenkirchen na Wattenscheid Mchg. Klaus Venjakob aliwatambulisha wageni hao kwa mkuu wa Mkoa na kueleza kusudi la kutembelea kwao. Kwamba majimbo ya Gelsenkirchen/ Wattenscheid na la K.K.K.T: Morogoro yamekuwa na urafiki na uhusiano kwa takribani miaka 30 iliyopita. Kwa muda wote huo pamekuwepo na utaratibu wa kutembeleana kati ya marafiki wa pande hizo mbili ili kujifunza hali za maisha na imani kwa Wakristo wao. Jambo la kushukuru ni kwamba urafiki na uhusiano kati ya majimbo hayo umekua na kuendelea vizuri.

Akielezea kwa ufupi Geographia ya jimbo, mkuu wa Jimbo hilo Mchg. Reginald Makule alisema lipo mkoa wa Morogoro na ni miongoni mwa mikoa iliyopanuka sana Tanzania wenye wakazi karibu 300.000. Idadi ya sharika za jimbo ni 13 zenye jumla ya Waumini/Wakristo 17.000.

Kwa kulinganisha tofauti za mikoa kati ya Gelsenkirchen na Morogoro, mkuu wa mkoa Frank Baranowski aliwaambia wageni kuwa “You are growing, we are shrinking” (Sie wachsen, wir schrumpfen), (Mnaongezeka, sisi tunapungua).  Na ndipo ulipoanza mjadala kati ya Ask. Mameo (53), Mkuu wa jimbo Mchg. Reginald Makule (51), Mchg. Paul Thomas (36), Norbert Mbwillo (45) na wawakilishi wanawake: Mama Lunyamadzo Gillah (43) na Natujwa Melau (49).

 Ask. Mameo alihitaji kujua ni changamoto zipi zinazosababisha mkoa wa Gelsekirchen upungue? Mkuu wa mkoa huo Frank Baranowski alijibu kuwa fedha zinazopatikana hazitoshi kabisa kukidhi haja mbalimbali mkoani humo na idadi ya wakazi wake ni wachache sana wenye hali na maisha ya kawaida. Pengine hali hii inaweza kuwa tofauti sana ukilinganisha umaskini uliopo kati ya nchi ya Ujerumani na Tanzania.

Wakiwa na hamu kubwa, wageni walihitaji kujifunza zaidi juu ya maisha ya pamoja na watu wenye dini na imani nyingine kwa mji wa Gelsenkirchen.  Na ndipo Mbwillo alipouliza: Inakuaje kwa mfano mtanzania mwislamu mwenye wake 4 anapokuja kuishi Gelsenkirchen? Msingi wa swali hilo umeonyesha kuwa pengine hali hiyo kwa Tanzania ni tofauti sana na Ujerumani. Mkuu wa mkoa alifafanua kuwa hakuna tofauti yoyote, kwani  tangu mwaka 1970, Waislamu wa kwanza kutoka Uturuki  waliingia na kuruhusiwa kuishi  nchini Ujerumani.

Mwisho wageni hao waliagwa kwa kupigiwa wimbo unaoelezea historia ya Schloss Horst takribani miaka 500 iliyopita. Kisha watanzania hao walimshukuru sana mwenyeji wao kwa mapokezi mazuri na kuimba wimbo wa kumshukuru  na kumsifu Mungu kwa ulinzi wake kwao.

Utaratibu wa ratiba yao mwishoni mwa juma ni:

-       Jumamosi, 15. Juni  saa 12 jioni wageni wote kushiriki ibada usharika wa Paul Gerhardt Horst, mtaa wa viwanda 38

-       Jumapili, 16. Juni wageni wakiwa kwenye vikundivikundi: Saa 3.30 asubuhi – Ibada usharika wa Apostel Buer, mtaa wa Horster 35; Saa 5.00 asubuhi – Ibada kwenye ukumbi wa Kanisa Markus, mtaa wa Biele 1 na Kanisa la Amani Schalke, mtaa wa Königsberger 120.

Imetafsiriwa na:

Mchg. Yordan Matandika

K.K.K.T: Dayosisi ya Morogoro