Heil und gesund gelandet - in Kisuaheli

Wageni kutoka Tanzania wawasili salama Gelsenkirchen

Baada ya safari ndefu, wamefurahi sana kukutana na marafiki zao wa jimbo la Gelsenkirchen na Wattenscheid. Pichani kutoka kushoto: Natujwa Melau, Mkuu wa jimbo Mchungaji Reginald Makule, Askofu Jacob Mameo, Mchungaji Paul Thomas, Mama Lunyamadzo Gillah na

Baada ya safari ndefu, wamefurahi sana kukutana na marafiki zao wa jimbo la Gelsenkirchen na Wattenscheid. Pichani kutoka kushoto: Natujwa Melau, Mkuu wa jimbo Mchungaji Reginald Makule, Askofu Jacob Mameo, Mchungaji Paul Thomas, Mama Lunyamadzo Gillah na Ndugu Norbert Mbwillo.

Siku ya Ijumaa, tarehe 7.6.2013, saa 1.40 asubuhi, wageni kutoka Morogoro Tanzania waliwasili salama uwanja wa Ndege wa Düsseldorf Ujerumani wakiwa na afya njema. Walipokelewa vizuri sana na wenyeji wao waliokuwa wakiwasubiri hapo uwanjani. Walisafiri na kufika Ofisi ya jimbo la Gelsenkirchen na Wattenscheid saa 5.00 asubuhi, baada ya kupata mzigo wao uliokuwa umepotea wakiwa safarini. Katika ofisi ya jimbo walipokelewa pia na umati mkubwa wa Wakristo kutoka sharika mbalimbali.

Sababu kubwa ya safari yao ni utaratibu uliokuwepo takribani miaka 30 iliyopita wa kutembeleana kati ya marafiki toka pande zote za majimbo ya Morogoro na Gelsenkirchen na Wattenscheid. Hii ni fursa pekee ya kukutana na Wakristo mbalimbali lakini pia kujadili mambo ya Kanisa kwa kudumisha uhusiano kati ya majimbo hayo.

Wageni hao ni pamoja na Askofu Jacob Mameo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Morogoro, Mchungaji Reginald Makule Mkuu wa jimbo la Morogoro, Mchungaji Paulo Thomas Mkuu wa pili jimbo la Morogoro, Ndugu Norbert Mbwillo Mhasibu jimbo la Morogoro, Mama Lunyamadzo Gillah, Mwenyekiti wa shule - Watoto yatima jimbo la Morogoro na Mama Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Wanawake wa jimbo hilo.

Walianza safari yao tarehe 6.6.2013 toka Morogoro umbali wa karibu Km 200 hadi Dar es Salaam hatimaye waliruka kwa Ndege massa 11 toka Dar es Salaam na kufika siku iliyofuata uwanja wa ndege wa Düsseldorf. Tofauti ya muda kati ya Morogoro na Gelsenkirchen kwa sasa ni saa 1. Inapotimu saa 6.00 mchana Gelsenkirchen, Morogoro ni saa 7.00 mchana.

Baadaye Mchungaji Klaus Venjakob, alisoma na kuwagawia ratiba juu ya mpango mzima wa mambo ya kufanya wakati wote wakiwa na wenyeji wao wa Gelsenkirchen. Kwamba kwa wiki la kwanza wataishi kwenye familia zifuatazo: Mchungaji Rüdiger Höcker na mkewe Eva, Bwana Franjo Kurth na mkewe Ursula, Dr. Andreas Schmidt na mkewe Sabine, Mchungaji Klaus Venjakob na mkewe Irene na Bwana Hans-Christian Wichlacz na mkewe Claudia.

Pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya mji wa Gelsenkirchen, wageni hao wamepewa fursa ya kuhubiri kila mwishoni mwa wiki.

Jumamosi, 8 Juni, saa 12.00 jioni wageni wote watashiriki Ibada katika usharika wa Stephanus Buer, mtaa wa Westerholter 92, Box 45894 Gelsenkirchen.
Jumapili, 9 Juni, saa 4.00 asubuhi kila wageni wawili watashiriki Ibada usharika wa Luther Hüllen, mtaa wa Flora 210, Box 45888 Gelsenkirchen, usharika wa Kreuze Leite, mtaa wa Gelsenkirchener 1, Box 44866 Bochum na saa 5.15 asubuhi kwenye ukumbi maalum (Chapel) Höntrop, mtaa wa Höntroper 35, Box 44869 Bochum.

Pia watamtembelea Mkuu wa Mkoa wa Gelsenkirchen, familia mbalimbali za mjini ambapo jioni moja watakutana na kujadiliana juu ya "ELIMU" katika shule ya pamoja ya Kilutheri, Gelsenkirchen-Bismark. Watapata nafasi ya kumtembelea Rais wa nchi ya Ujerumani na mlima uliotengenezwa kwa vitu vya asili Bochum.

Siku ya Jumatano, 19 Juni, kutakuwa na sherehe fupi ya kuwaaga wageni katika usharika wa Horst kabla ya kurudi kwao Tanzania.

Imetafsiriwa na: Mchungaji Yordan Matandika
                          K.K.K.T: Dayosisi ya Morogoro

Ein starkes Stück Kirche!

Presbyterinnen und Presbyter erzählen von ihrer Arbeit

Kirche für alle

Paare, die ihre Liebe unter Gottes Segen stellen möchten, sind bei uns willkommen.

Diakonie

Unser Diakoniewerk heilt und berät, hilft und begleitet Menschen durch ihr ganzes Leben. Die Evangelischen Kliniken Gelsenkirchen gehören ebenso dazu wie Diakoniestationen und Beratungsdienste.

Telefonseelsorge

Die Telefonseelsorge ist rund um die Uhr für Sie da.